Halmashauri ya Wilaya Kibiti itafikia malengo/matarajio iliyojiwekea kwa;-
kushirikisha Jamii katika kubuni, kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini Miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwenye ngazi zote na kuhakikisha kuwa inaweka mikakati endelevu ya ukusanyaji wa mapato, ambayo yatatumika kwa uangalifu na umakini wa hali ya juu ili yaweze kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi.
Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti pia itaelimisha jamii kuhusu Sera mbalimbali za Kitaifa na umuhimu wa kutumia sheria ndogo zilizopo kuhakikisha kuwa shughuli zote zinazotekelezwa kwenye maeneo yao, zinafanyika kulingana na taratibu, kanuni na sheria zilizopo.
Kushirikisha jamii katika kutekeleza miradi kwa nguvu zao wenyewe kwa njia mkabala bila kuathiri hali zao kiuchumi na kufikia malengo ya kuongeza wigo wa kutolea huduma za kijamii kama afya, elimu, uzalishaji na utawala bora.