Majukumu ya Idara ya Ardhi na Maliasili
• Kuratibu uandaaji wa Mipango ya kimbinu ya kuendeleza Miji (Strategic Urban Development Plan).
• Kuratibu uandaaji wa mipango ya maeneo yaliyoendelezwa kiholela.
• Kuandaa michoro ya mipangomiji.
• Kutoa masharti ya uendelezaji wa Ardhi.
• Kupokea michoro ya Mipangomiji na taarifa za maeneo ya ardhiyanayopendekezwa kuiva kwa ajili ya uendelezaji kimji.
• Kuchambua takwimu na taarifa kwa ajili ya maandalizi ya mipangomipya ya makazi.
• Kupokea na kuweka kumbukumbu za maombi ya mabadiliko ya matumizi ya ardhi na umegaji wa viwanda.
• Kuhakikisha kwa mabadiliko ya matumizi ya ardhi yanaingizwa katika michoro.
• Kusimamia/Kuthibiti uendelezaji wa makazi.
• Kuratibu uandaaji wa mipango shirikishi ya matumizi bora ya ardhi ya vijiji.
• Kutoa ushauri wa uendelezaji wa ardhi kwa wananchi.
• Kukagua kazi za Upimaji.
• Kupima maeneo mbalimbali (Mashamba na viwanja).
• Kuandaa michoro kwa ajili ya Hatimiliki za kisheria.
• Kutunza kumbukumbu za Upimaji.
• Kurudisha mipaka.
• Kuhifadhi na Kutunza Misitu na Mazingira.
• Kuhimiza na kusimamia upandaji wa miti na kutunza misitu vijijini.
• Usimamizi, ulinzi na utunzaji wa misitu na rasilimali zake.
• Usimamizi wa sheria za Misitu.
• Kusimamia, na kufuatilia makusanyo na ushuru wa mazao ya misitu.
• Ulinzi na usimamizi wa vyanzo na kinga za maji, utunzaji wa udongo na ulinzi wa mimea.
• Kusimamia hifadhi za misitu na kutoa elimu kwa jamii.
• Kusimamia shughuli zote za ufugaji nyuki vijijini.
• Kutunza mazingira ya nyuki yaliyopo pamoja na kupanda miti ifaayo kwa nyuki.
• Kuhamasisha na kueneza kwa jamii na wanavijiji kufuga na kutunza nyukii kisasa.
• Kuhamasiha jamii kutengeneza mizinga ya kisasa ya gharama nafuu kwa kuzingatia mazingira yao
• Kuunda na kusimamia vikundi vya ufugaji nyuki vijijini.
• Kusimamia mazao ya ufugaji nyuki.
• Kutoa elimu kwa jamii kuhusu ufugaji nyuki wa kisasa huko vijijini.
• Kuhamasiha watu binafsi taasisi mbalimbali kufuga nyuki kwa lengo la kujiongezea kipato na lishe.
• Kutunza mazingira na wanyamapori.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.