Kutoa ushauri wa kisheria kwa Halmashauri pale itakapohitajika kufanya hivyo au itakapoonekana kuna umuhimu wa kushauri juu ya suala lolote la kisheria katika Halmashauri.
Kuhudhuria vikao vya kisheria vya Halmashauri, vikao vya Wakuu wa Idara,kamati za kudumu za Madiwani na Baraza kuu la Madiwani.
Kushughulikia mafaili mbalimbali yanayoletwa katika kitengo cha sheria yakihitaji kufanyiwa kazi.
Kuandaa taarifa za kila robo ya mwaka za shughuli zilizofanyika katika kitengo kwa kipindi husika.
Kupitia fomu mbalimbali za Mikopo ya Watumishi.
Kufanya usimamizi na kusimamia utendaji kazi wa Mabaraza ya kata katika Halmashauri.
Kuhudhuria mafunzo mbalimbali ndani na nje ya Wilaya yatakapokuwa yametokea.
Kupitia mikataba mbalimbali ni kuifanyia Approval kabla ya kusainiwa na Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Halmashauri.
Kuandaa nyaraka mbalimbali za kesi zilizopo Mahakamani.
Kuandaa mikataba mbalimbali inayohusu Halmashauri pale itakapohitajika kufanya hivyo.
Kushirikiana na Mtunza Hazina wa Halmashauri katika kushughulikia masuala mbalimbali ya kisheria katika shughuli nzima za ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.
Kuandaa rasimu mbalimbali za sheria ndogo za Halmashauri zinazotakiwa kutungwa na kusimamia upitishaji wake katika mamlaka mbalimbali.
Kushiriki na kufanya utatuzi wa migogoro mbalimbal iya kisheria katika Halmashauri.
Kusimamia utekelezaji wa sheria ndogo ndogo za Halmashauri katika ngazi mbalimbali ndani ya Halmashauri.
Kusaidia mamlaka za vijiji katika kutunga sheria Ndogondogo za vijiji vyao na kuwasaidia kuandaa mikataba mbalimbali ya utekelezaji wa shughuli za miradi mbalimbali katika maeneo yao.
Kufanya tafiti mbalimbali za kisheria (legal Research) kwa kesi mbalimbali zilizopo Mahakamani.
Kufanya majukumu mengine mbalimbali kama yatakavyokuwa yameelekezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo.
Katibu wa kamati ya Ukaguzi ya wilaya (Audit Committee).
Kuvisaidia vijiji katika masuala mbalimbali ya kisheria yahusuyo vijiji vyao.