Majukumu ya Idara ya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana;
Idara ina majukumu yafuatayo;
Kuhamasisha jamii katika suala zima la kuondoa umaskini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Maendeleo ikiwemo Serikali, Wahisani pamoja na Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs).
Kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa sera ya Maendeleo ya Jamii katika ngazi mbalimbali za jamii kuanzia vijiji, kata na Halmashauri.
Kuhamasisha jamii kuachana na mila zenye kuleta madhara na zinazokinzana na haki za binadamu ili kuleta maendeleo endelevu kwa jamii.
Kuhamasisha jamii juu ya hifadhi ya mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Kuijengea jamii uwezo hususani makundi maalum (wanawake, watoto,wazee na wenye mahitaji maalum) ili waweze kumiliki uchumi kupitia rasilimali zilizopo.
Kutoa elimu ya ujasiliamali kwa vikundi vya wanawake na vijana pamoja na kutoa mikopo midogo midogo yenye riba nafuu ikiwa na lengo la kuongeza mitaji na kukuza uchumi kwa vikundi vya ujasiliamali.
Kuelimisha jamii juu ya mapambano dhidi ya UKIMWI na kupunguza kasi ya maambukizi mapya ya VVU/UKIMWI.
Kushirikisha jamii katika kupanga, kutekeleza, kusimamia na kutathmini shughuli za maendeleo.