Hayo yamesemwa leo katika kikao na Walimu Sambamba na Viongozi wa Chama Cha Walimu Wilaya pamoja na Baadhi ya Walimu waliokuja na Chama kipya cha Walimu CHAKUWAWATA ambapo amewataka kuweza kufata taratibu za uanzishwaji wa chama kutoka ngazi ya Taifa,Mkoa hadi wilaya.
Aidha Mhe.Kolombo aliendelea kusisitiza walimu waweze kufanya kazi ambazo wameajiriwa nazo na kuwasilikiliza viongozi wao ngazi kwa ngazi ili waweze kuwa na utumishi bora kipindi chao chote cha Utumishi wa Umma na kuwa na usalama kazini.
Sambamba na hayo Mwanasheria wa Halmashauri ya Kibiti ndugu.Rajabu Mwinyi aliendelea kuwafahamisha ya kuwa Kuna taratibu za Kufata pindi unapotaka Kuanzisha Chama cha wafanyakazi Hivyo Msisitizo Mkubwa ni ufatwaji wa Sheria,Kanuni na Miongozo Mbalimbali ya Utumishi wa Umma pia kuhusisha Vyombo vinavyo simamia Utumishi wa Umma.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.