Katibu wa Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kibiti Ndugu.Eliasa Kitasa kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Kibiti Mhe.Twaha Ally Mpembenwe Juni 26,2025 ameongoza hafla fupi ya makabidhiano ya gari jipya la wagonjwa katika kituo cha afya Nyamatanga kilichopo katika kata ya Ruaruke.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano Ndugu Eliasa amesema ujio wa gari hilo utasaidia kupunguza changamoto za usafiri kwa wagonjwa na wananchi wa kata ya Ruaruke kwa ujumla.
Naye Diwani wa kata ya Ruaruke Mhe.Riziki Ndambwe ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kibiti kwa kufanikisha ujio wa gari hilo katika kata ya Ruaruke
"Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe Dkt.Samia Suluhu Hassan lakini pia ofisi ya Mbunge wetu Mhe.Twaha Ally Mpembenwe kwa kutuletea gari hili katika kata yetu "
Aidha amewataka wataalamu wa afya wa kituo cha Nyamatanga kuhakikisha wanalitumia gari hilo katika matumizi sahihi ili iwe msaada kwa wakazi wa kata hiyo.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.