31 DISEMBA MWISHO WA ZOEZI LA UANDIKISHWAJI ELIMU YA MSINGI.
4755 WAANDIKISHWA DARASA LA KWANZA NA 2365 ELIMU YA AWALI
Ikiwa imesalia siku moja ya kufungwa kwa zoezi la uandikishwaji wa watoto waliofika umri rika wa kuanza darasa la kwanza na elimu ya awali katika Wilaya ya Kibiti Mkurugenzi Mtendaji Mohamed Mavura ameendelea kuwakumbusha wazazi na walezi wote kuhakikisha watoto wao wameandikishwa.
Kwa mujibu wa takwimu za zoezi la uandikishwaji kutoka Idara ya Elimu ya Msingi,mpaka 29/12/2022 jumla ya watoto 4755 wameandikishwa Sawa na asilimia 96 kati yao ME 2376 na KE 2379 ambapo awali waliweka lengo la kuwafikia watoto 4932 kati ya walioandikishwa 14 ni watoto wenye uhitaji maalum.
Vile vile Kwa upande wa Elimu ya awali jumla ya watoto 2365 wameandikishwa ikiwa ni sawa na asilimia 104 kati yao ME ni 1119 na KE ni 1246,ambapo awali walikusudia kuandikisha watoto 2269.
Aidha ili kufika malengo Walimu na Viongozi wa ngazi ya Kata, kitongoji na Kijiji wamekuwa wakipita nyumba kwa nyumba kuhakikisha wanaandikisha watoto na zoezi linakamilika kama ilivyoelekezwa.
Hayo yamebainishwa na Afisa Taaluma Msingi Hamis Athuman Shemahonge katika tathmini ya kufuatilia uandikishaji huku akisema uandikishaji unakwenda vizuri na kazi inaendelea.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.