Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti imekabidhi pikipiki moja kwa Afisa msaidizi wa Kilimo Kata ya Mtunda Stanley Kusaga kwa lengo la kudhibiti utoroshaji wa mazao, kurahisisha ufuatiliaji na uzalishaji wa mazao yaliyo bora.
Akikabidhi pikipiki hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Afisa kilimo na Ushirika Wilaya ya Kibiti Bwenda Bainga amesema, pikipiki hiyo itatumika kwa ajili ya kutembelea wakulima na kufundishwa kanuni bora za kilimo ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.
Vilevile Bainga amesema pikipiki hiyo kwa upande mwingine itatumika kudhibiti utoroshaji wa mazao Kwenda maeneo ya Jirani kwa kufanya doria katika maeneo mbalimbali ya mipaka ya wilaya .
Aidha Bainga ametoa angalizo kwa Afisa kilimo kwamba pikipiki hiyo ikatumike kama ilivyokusudiwa na si vinginevyo kama matumizi ya shughuli binafsi na bodaboda kwani itakuwa ni kinyume na maelekezo ya Halmashauri na hatua kali zitachukuliwa.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.