JUMLA YA TSH. MIL. 550 ZATUMIKA KUKAMILISHA UJEZI HUO.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Meja Edward Gowele amezindua kituo cha Afya Mjawa katika Kata ya Mjawa chenye thamani ya mil. 550 Kwa fedha za Tozo za Miamala ya simu na Mapato ya ndani.
Meja Gowele ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika uzinduzi huo amesema kituo hicho kitunzwe na kulindwa kwani fedha zilizotumika kukamilisha Ujenzi huo ni nyingi huku akimshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyotekeleza Ilani ya chama Tawala kwa kuhakikisha anatoa fedha za Miradi ya afya n.k.
“Nimezindua rasmi kituo cha afya Mjawa, kiko tayari kutoa huduma kwa wananchi” alisema Gowele huku akisisitiza wananchi kujiunga na mifuko ya bima ya afya ya NHIF na CHIF ambayo itarahisisha kupata huduma kwa haraka ikiwa ni pamoja na kupata huduma ya dawa na vipimo.
Akiwa kituoni hapo Gowele amewataka wahudumu wa kituo hicho kuwahudumia wananchi kwa moyo wa kujitoa huku akisisitiza jamii husika kushirikiana na watumishi hao wapya kwani ni bahati ya kipekee kituo kufunguliwa na kupata watumishi.
Vile vile Gowele ameziagiza Taasisi za TARURA, TANESCO na KIBUWASA kuhakikisha huduma ya miundombinu ya barabara, umeme na maji zinapatikana kwa haraka ili kuimarisha na kurahisisha huduma zinazotolewa katika kituo hicho na atarudi kuja kukagua kama changamoto hizo zimemalizika .
Awali kaimu Mkurugenzi Mtendaji Denis Kitali ameishukuru kamati ya ulinzi na usalama kwa namna inavyokuwa mstari wa mbele kufuatilia Miradi inayoendelea sambamba na kumshukuru Mhe.Rais kwa kutoa fedha nyingi za kutekeleza Miradi ya maendeleo katika Afya, elimu n.k hususani Wilaya ya Kibiti kwa namna ilivyobahatika.
Aidha Mganga Mkuu wa Wilaya Daktari Elizabeth Oming’o wakati akitambulisha watumishi wa idara yake ambao miongoni mwao 6 ni wa ajira mpya ameishukuru serikali ya Mama Samia na uongozi wa Wilaya kwa ujumla kwa kutoa fedha za Miradi sambamba na usimamizi mzuri mpaka sasa kituo cha afya kimezinduliwa rasmi kuanza kutoa huduma kwani haikuwa kazi rahisi.
Naye Diwani wa kata ya Mjawa Mhe Ramadan Chepa ametoa shukrani Kwa uongozi wote kuanzia ngazi ya Rais,Mhe Mbunge,kamati ya ulinzi na usalama Mkurugenzi mtendaji na Wataalam wake kwa juhudi zilizofanyika kuhakikisha kituo cha afya Mjawa kinaanza kutoa huduma kuwa ni faraja kubwa kwa wananchi wa Mjawa . Kwa nyakati tofauti Mwenyeji wa huduma za jamii na Diwani wa Kibiti Hamidu Ungando, mtendaji wa kata ndg Abeid Ponsa,na mwenyekiti wa Jaribu mpakani Bakari Msanga wote kwa pamoja wanetoa shukrani zao za pekee Kwa kupatikaka Kwa huduma ya afya Mjawa na viunga vyake, huku wakishururi serikali kwa namna ilivyowaona Kwa jicho la pekee kuwapelekea mradi huo na Sasa umezinduliwa rasmi tayari Kwa kutoa huduma.
#Kazi iendelee…
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.