Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo akiwa na Katibu Tawala Bi Maria Katemana amezindua kampeni ya Matone ya vitamin A na dawa Kinga za minyoo ambayo itatolewa katika vituo vyote vya Afya kwa muda wa mwezi mzima kwa watoto wenye umri wa miezi 6 -59 (chini ya miaka 5).
Katika hafla hiyo iliyofanyika katika Kituo cha Afya Kibiti Kanali Kolombo amesema Serikali ilipokea chanjo hizi nchini ili wananchi waweze kujikinga na maradhi yanayoweza kulipuka lengo kuu likiwa ni kuhakikisha kunakuwa na jamii yenye Afya Bora .
Hata hivyo amewapongeza kinamama na kinababa waliojitokeza kupeleka watoto wao huku akisisitiza wakitoka hapo wakahamasishe wenzao ambao hawajawapeleka watoto wao kupata huduma hiyo muhimu.
"Chanjo ambazo zimeshatolewa nchini ni kama polio, ndui, surua, COVID 19 , homa vya ini n.k na baada ya chanjo hizo kutolewa kuna baadhi ya maradhi yaliweza kupotea kabisa "Alisema.
Aidha Afisa lishe wa Wilaya ya Kibiti Bi. Roina Dazo amesema Vitamini A ni kirutubisho muhimu kwa ukuaji wa ngozi na uadilifu, hususani katika utendakazi wa kinga, ukuaji wa mifupa, ukuaji wa kiinitete katika mwili wa binadamu n.k
Vilevile kwa upande wa dawa za minyoo amesema, zinasaidia kumlinda mtoto dhidi ya upungufu wa damu, zinaleta hamu ya kula na pia zinazuia kupungua kwa uzito na zinaboresha Afya ya mtoto.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.