10.11.2023
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Bw Hemed Magaro akiwa ameambatana na wataalam wa Halmshauri hiyo wamefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo yenye thamani ya sh 365,761,976.04 ambayo inatekelezwa kwa fedha za mapato ya ndani na sanitation ili kukamilisha majengo mapya na ukarabati kwa yale ya zamani
Miradi iliyokaguliwa ni ya ujenzi wa matundu ya vyoo, madarasa, vichomea taka, sehemu za kunawia na zahanati katika kata za dimani, Kibiti, mchukwi, Ruaruke, Mtawanya, Bungu na Mjawa na Mlanzi.
Katika ziara hiyo, Bw. Magaro amewaagiza mafundi kuongeza kasi ya majenzi na kuzingatia ubora, huku akiwaagiza wasimamizi wa miradi hiyo kusimamia kikamilifu na kuhakikisha miradi yote inakamilika ifikapo disemba mosi kwani hakutakuwa na muda wa nyongeza.
Hata hivyo Mkurugenzi Magaro amewasisitiza wasimamizi hao wa miradi kuhakikisha nyaraka zote zinakuwepo kwa kufuata maelekezo ya manunuzi na mkaguzi wa ndani jambo litakalowasaidia kuepuka mikanganyiko ya hapa na pale.
Mbali na hayo Bw. Magaro amewaelekeza wasimamizi wa mradi kuhakikisha kila fundi aliyepewa kazi anakuwa na mkataba wa kazi ambao watawekeana makubaliano.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.