Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kibiti Bw. Hemed S. Magaro amemtangaza Bw. Hamada J. Hingi wa CCM kuwa mshindi wa Udiwani kata ya Mahege, iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti.
Bw. Hingi Amepata kura 928 kati ya Kura halali 1088 zilizopigwa katika uchaguzi huo , Jumla ya Wagombea 6 walijitokeza kugombea nafasi hiyo ya Udiwani Kata ya Mahege ambapo Bw. Mrisho M. Jongo wa CUF alipata kura 133, Mzuzuri N. Sadick wa NRA aliyepata kura 03, Mussa J. Maramuah wa UDP aliyepata kura 12, Seif M. Mkokwa wa UMD aliyepata kura 6 na Sultan S. Mpondi wa UPDP aliyepata kura 6.
Aidha Bw. Magaro Alisema kwamba jumla wapigakura waliojiandikisha ni 4352, idadi halisi ya wapiga kura ni 1118, idadi ya kura halali ni 1088na idadi ya kura zilizoharibika 30.
Hata hivyo mara baada ya matangazo kutangaza baadhi ya vyama shiriki vya upinzani vya CUF na UPDP wamekiri uchaguzi kwenda salama, na kukubali matokeo kuwa mgombea Hamada Hingi amewashinda katika kinyang'anyiro Cha uchaguzi huo.
"Uchaguzi huu ni wa kipeee, haikuwa na makandokando Wala fujo" Walisema wapinzani hao.
mwisho Viongozi wa tume ya Taifa ya uchaguzi wamepongeza namna uchaguzi ulivyofanyika ukiwa na maandalizi yaliyojitosheleza.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.