15.2.2024
Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo amekabidhi magari mawili aina ya Toyota Hilux yenye thamani ya Sh. 199,896,600/=. Kati ya hizo Sh. 190,000,000/= ni fedha kutoka Serikali kuu na Sh. 9,896,600/= ziliongezewa kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti.
Magari hayo yanakwenda kutumiwa na Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu na lingine linakwenda kutumiwa na Idara Ujenzi.
Akikabidhi magari hayo Kanali Kolombo amemshukuru Mhe. Rais Dkt. SSH na Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti kwa kufanikisha magari hayo kupatikana kwani yanakwenda kurahisisha majukumu ya kiutendaji ndani ya Wilaya.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Ndg. Hemed Magaro amesema kupatikana kwa magari hayo mawili kukutasaidia kurahisisha shughuli za Idara husika zinazopokea magari hayo hususani Idara ya Ujenzi kufika kwenye miradi mbalimbali kwa haraka kutoa huduma tofauti na ilivyokuwa awali.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti ambaye ni Diwani wa Kata ya Bungu Mhe. Ramadhani Mpendu mara baada ya upokezi wa magari hayo amezitaka Idara zilizokabidhiwa magari hayo kuyatumia vizuri ili yaweze kudumu na kufanya kazi iliyokusudiwa.
Akitoa shukrani kwa niaba Mbunge wa Jimbo la Kibiti Diwani wa Kata ya Mtawanya Mhe. Malela Tokha amesema Mhe. Mpembenwe anamshukuru sana Mhe. Rais wa awamu ya sita Dkt. SSH kwa kuikumbuka na kujali Wilaya ya Kibiti lakini kipekee amempongeza Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Hemed Magaro na timu ya walaalam wake kuona umuhimu wa kuongeza fedha za mapato ya ndani jambo lililopelekea kufanya ununuzi wa magari hayo mawili.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.