Ujenzi wa Jengo la wagonjwa wa dharula (EMD)katika Hospitali ya Wilaya ya KIBITI ni neema kwa wakazi wa wilaya ya kibiti na viunga vyake kwani ni suluhisho la kupata huduma za haraka pindi Inapotokea dharula za ugonjwa kwa wananchi.
Akizungumzia mradi huo unaodhaminiwa na serikali kuu kwa fedha za uviko 19 jumla ya sh.mil 300 ,Mganga mfawidhi Dr. Chagi Jones Lymo amesema mradi utasaidia kupunguza vifo vinavyotokea kwa asilimia kubwa kwa kuchelewa kupata huduma ya haraka pindi zinapotokea.
Vileile Lymo amefafanua kwamba kupitia mradi wa jengo hilo la dharula watakaopata huduma za haraka katika hospital hiyo ni wale waliopata ajali,upasuaji wa haraka na wagonjwa wengine wa magonjwa mbalimbali ya ndani.
Kwa upande wa faida zitokanazo na mradi huo katika Wilaya ya kibiti ni pamoja na kuimarisha na kuongeza ufanisi wa utendaji katika idara ya Afya kwani dhumuni la mradi ni kumsaidia mgonjwa wa dharula kwa haraka na bila usumbufu .
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.