MKOA WA KIPOLISI RUFIJI WATOA VIFAA VYA USAFI.
NI KATIKA KITUO CHA AFYA KIBITI.
Jeshi la Polisi nchini Kanda maalum Mkoa wa kipolisi Rufiji limetoa msaada wa vifaa vya kufanyia usafi na kufanya usafi wa Mazingira katika kituo cha afya kibiti ikiwa ni utaratibu wa kawaida katika jeshi kama walivyoelekezwa ambapo kila mkoa umeshiriki zoezi hilo katika maeneo yao.
Akikabidhi vifaa hivyo Kamishna Msaidizi wa Polisi Mkoa wa kipolisi Rufiji Protas Bigeyo Mutayoba (RPC) amesema vifaa vilivyotolewa ni mchango wa jeshi hilo kuonyesha ushirikiano katika mpango wa ushirikiswaji jamii kuondoa uharifu nchini na ni alama ya kuwa kitu kimoja.
“Leo tumechagua kuja kibiti kituo cha afya kushiriki zoezi la usafi Kwa kufyeka nyasi, kukatia miti kulimia njia tunaweka ukaribu na jamii”alisema Kamishna Mutayoba.
Vifaa vilivyotolewa kituoni hapo ni mifagio 29 ya kufagilia nje, ndoo za kudekia 9, mifagio 9 ya kufagilia ndani na mifuko 2 ya sabuni ya unga Kwa ajili ya kufulia .
Utaratibu huo ni wa kawaida ambao hufanyika angalau mara moja kwa mwaka zoezi hilo la usafi limeshirikisha jumla ya askari 82 ambao kati yao ni askari 57,wakaguzi 10 na maofisa 15 wote wakitoka katika wilaya za Rufiji, kibiti na Mkuranga ambapo mafia hawakuweza kushiriki kutokana na jiografia ya eneo husika na hali ya hewa.
Vilevile Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Daktari Elizabeth Oming’o amelishukuru jeshi la Polisi Kwa msaada walioutoa, kwa namna walivyojitoa kufanya usafi wa Mazingira kwani wameonyesha kujali, kituo cha afya kibiti ni Kituo kikubwa kinachohudumia watu wengi hivyo kinapaswa kuwa na Mazingira safi muda wote.
Aidhaa Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya kibiti Daktari Beatrice Malekela amelishukuru jeshi hilo pia kwa ushirikiano waliouonyesha kwani ni sehemu ya kuimarisha Utendaji katika Taasisi hizo ambazo Kwa ujumla zinategemeana kiutendaji katika Ujenzi wa Taifa.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.