15 Nov, 2023
Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya wilaya ya Kibiti imetembelea miradi 10 ya Maendeleo inayotekelezwa katika kata 5 ndani ya halmashauri hii (Kibiti, Mchukwi, Mjawa, Bungu na Mtawanya) kwenye kipindi cha robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Miradi iliyokaguliwa ni ujenzi wa shule mpya, matundu ya vyoo, madarasa, nyumba ya watumishi, vichomea taka na sehemu za kunawia mikono. Thamani ya miradi hiyo ni shilingi 921,471,122.00 ambazo ni fedha zilizotokana na Mapato ya ndani ya hamashauri, Sanitation, SEQUIP na EP4R.
Mwenyekiti wa kamati pamoja na wajumbe wameridhishwa na maendeleo ya miradi hiyo isipokuwa mradi mmoja wa ujenzi wa nyumba ya watumishi Jaribu Mpakani ambapo Mkandarasi ametakiwa kufanya marekebisho kwenye baadhi ya kuta pamoja na renta.
Aidha Mwenyekiti pamoja na wajumbe wa kamati wamesisitiza wakandarasi pamoja na mafundi wa ndani kufanya kazi kwa kasi na ubora wa juu huku wakifuata taratibu zote, kanuni na miongozo. Kwa upande mwingine wanakamati wamemtaka Mkandarasi wa Halmashauri kuwa karibu zaidi na mafundi hao ili kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa usahihi na kwa wakati.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.