Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango tarehe 27/04/2021ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Ramadhani Mpendu ilifanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo pamoja na vikundi vya ujasiliamali ambavyo vilipatiwa mikopo na Halmashauri ikiwa ni takwa la kisheria la kutoa asilimia kumi(10%) ya makusanyo ya mapato yake ya ndani, ni utaratibu wa kawaida kwa kamati hiyo kutembelea miradi kila baada ya robo mwaka.
Miradi minne(4) ilitembelewa ikiwa ni ujenzi wa madarasa mawili na matundu manne ya vyoo shule ya msingi Bungu’A’ ambayo walipata ufadhili toka Songas,Ujenzi wa madarasa matatu na ofisi ya walimu shule ya msingi Mangombela pia walipata ufadhili toka Songas,Ujenzi wa chumba cha maabara shule ya sekondari Mtawanya kwa fedha ya mapato ya ndani,Ujezi wa wodi tatu ya wanaume,wanawake na Watoto hospitali ya Wilaya kwa ruzuku toka Serikali kuu pamoja na vikundi viwili vya ujasilia mali cha wanawake Kijiji cha Motomoto ambacho kilipatiwa kiasi cha shilingi milioni tatu(3,000,000/=) awamu ya pili kwa shughuli za kilimo cha ufuta na kikundi cha bodaboda ‘Terminal’ kilichopatiwa shilingi milioni ishirini na mbili(22,000,000) kwa ajili ya ununuzi wa Bajaji tatu(3) fedha hizi zilitolewa na Halmashauri kutoka kwenye mapato yake ya ndani.
Kwenye ziara hiyo kamati ilirizishwa na maendeleo ya hatua zilizofikiwa za ujenzi wa miradi yote na kupongeza wataalam kwa usimamizi mzuri.
Kamati ilifurahishwa sana na ushiriki wa wananchi wa Kata ya Bungu kwa moyo wa kujitolea kwenye kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za kijamii zinazofanyika kwenye kata yao.”Natoa pongezi kwa Wananchi wa Bungu kwa moyo mkubwa wa kujitolea wanao uonyesha kwani kiasi cha fedha walichopatiwa na wafadhili kilikuwa kidogo ukilinganisha na kazi kubwa iliyofanyika NAWAPONGEZA SANA” pongezi hizi zilitolewa na makamu mwenyekiti Mhe.Omari B. Twanga kwa niaba ya kamati.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.