KAMATI YA FEDHA,UONGOZI NA MIPANGO YATEMBELEA KIWANDA KIDOGO CHA KUTENGENEZA SABUNI ZA KUFULIA NA KUOSHEA VYOMBO KIBITI.
Leo tarehe 26.10.2021 kwenye ukaguzi wa miradi robo ya kwanza kamati ya Fedha,Utawala na Mipango imetembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti.
Miradi iliyotembelewa ni Ukarabati wa Zahanati na ujenzi wa nyumba ya mganga Mchukwi kiasi cha shilingi 48,000,000/=fedha iliyotolewa na wahisani(RBF),Ujenzi wa kituo cha afya Mjawa shilingi 250,000,000/= fedha iliyotolewa na serikali kuu(Tozo ya miamala ya simu),Ujenzi wa banda la kupumzikia abiria kituo cha basi Kibiti 20,000,000/= fedha ya mapato ya ndani pamoja na kikundi cha wanawake wajasilia mali wanaujulikana kama MKOMBOZI GROUP ambapo walipatiwa kiasi cha shilingi 19,869,972/= toka kwenye asilimia kumi ya Wanawake,Vijana na watu wenye ulemavu.
Kikundi hiki cha wajasilia mali kina jumla ya wanachama watano ambao waliungana na kuamua kuanzisha kiwanda kidogo cha kutengeneza sabuni zinazojulikana kama KIBITI SOUP.
Aidha,baada ya kutembelea kiwanda hicho mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Ramadhani Mpendu pamoja na wajumbe wenzake wa kamati ya fedha waliwapongeza wanawake hao kwa kuthubutu kuanzisha kiwanda hicho na kuwashauri kujitangaza zaidi ili kupata soko la uhakika, katika kuunga jitihada zao mwenyekiti wa Huduma za jamii ambaye pia ni diwani wa Kata ya Kibiti Mhe. Hamidu Ungando alisema yeye anatumia sabuni hizi na kila anapofanya vikao mbalimbali anakwenda na sabuni zao ili kuzitangaza na kuwatafutia soko.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.