Mkuu wa wilaya ya kibiti Kanali Joseph Kolombo amewaagiza Viongozi wote kuanzia ngazi ya mitaa kuhakikisha wanatokomeza na kufuatilia changamoto za ukatili wa kijinsia katika maeneo yao pindi yatokeapo au panapokuwepo na viashiria hivyo.
Kanali amebainisha hayo katika Kilele cha maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Duniani yalifofanyika kituo cha mabasi kibiti, yaliyobeba kauli mbiu inayosema ( kuelekea miaka miaka +30 ya Beijinig chagua kutokomeza ukatili wa kijinsia).
Akisoma taarifa Bi. Agatha Lema kutoka Shirika la msaada la Norway chini ya kanisa KKKT (NCA) amesema ukatili wa kijin sia ni suala ambalo linaathiri jamii wahanga wakiwa wanawake, wanaume na watoto kwa asilimia kubwa kama vile vipigo, ubakaji, unyanyasaji wa Kingono, kijinsia n.k
Aidha amesema kupitia shirika hilo wamekuwa wakitekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia IR VIKOBA, utawala bora, pamoja na elimu nadharia kama vile utengenezaji wa sabuni, batiki, ufugaji wa kuku na nyuki jambo linalowawezesha kujikwamua kiuchumi na kuepukana na utegemezi.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibiti Mhe. Twaha mpembenwe amesema kuna kila sababu ya kuhakikisha ukatili wa kijinsia unakomeshwa kwani unachangia kuchelewa kwa maendeleo kutokana na rasilimali watu kupotea.
Naye Diwani wa Kata ya Kibiti Mhe. Hamidu Ungando kwa niaba ya Mwenyekiti wa Halmashauri ameishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kuwa na vituo vya kutoa msaada kwa kisheria kwa wananchi wasiojiweza huku akipongeza Taasisi za dini kwa mashirikiano mazuri.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.