Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Mhe.Kanali.Joseph Kolombo amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua kazi kubwa na mchango wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika jamii.
Kanali Kolombo ameyasema hayo wakati akifungua Kongamano la Mashirika yasiyo ya Kiserikali lenye lengo la kutathmini shughuli zinazotekelezwa na mashirika kwa mwaka husika na kukumbushana masuala mbalimbali ya kiutendaji
‘’Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti inatambua mchango wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika maendeleo na ustawi wa jamii.Mashirika yasiyo ya Kiserikali yamekuwa na mchango mkubwa katika masuala ya mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, utunzaji wa mazingira,udhamini katika elimu, ulizni na ustawi wa wanawake na Watoto Pamoja na msaada wa kisheria’’
Aidha ameongeza kuwa katika kuimarisha dhana ya uwazi na uwajibikaji wa Mashirika, Serikali ilizindua Mwongozo Mpya wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali wa mwaka 2024 ambao utasaidia kuweka mazingira wezeshi kwa Mashirika yasiyo ya Kiserikali na kukuza ushirikiano baina ya Mashirika na Wizara yenye dhamana, Taasisi za Kiserikali, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mita ana Sekta binafsi.
Sambamba na hayo Mkuu wa Wilaya pia amezindua Mwongozo huo Mpya wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali wa Mwaka 2024.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.