7.3.2024.
Katika kuhitimisha Juma la Elimu Wilaya ya Kibiti majira ya alasiri kumefanyika michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mchezo wa mpira wa kikapu ,mpira wa miguu pamoja na mpira wa Pete, michezo ambayo ilishuhudiwa na wadau mbalimbali wa elimu wakiongozwa na walimu na wanafunzi.
Katika Tamasha hilo timu ya mpira wa pete ya Kibiti Queens imeongoza kwa ushindi wa magoli 18 dhidi ya JKT MKUPUKA ambao kinyonge walijitutumua na kuambulia magoli 6 pekee wakiwa katika viunga vya uwanja wa shule ya Sekondari ZIMBWINI.
Mpira wa kikapu nao ulichezwa katika viunga hivyo hivyo ambapo Kibiti Worriors iliibuka kidedea baada ya kuonyesha utaalam wa kudanki kwa ushindi wa alama 70 na kuwanyamazisha Kibiti boys ambao walipata alama 50.
Kwa upande wa mpira wa miguu , kabumbu limepigwa kwenye Uwanja wa Samora na mpaka mpira unakwisha wafunga buti wa JWTZ KINYANYA wameshindwa kufurukuta na kuchabangwa magoli 4 kwa nunge dhidi ya KURUGENZI FC.
Sherehe ya Juma la Elimu ilinogeshwa na burdani nyingine kama vile, kwaya, ngonjera, shairi, muziki, Ngoma , vichekesho n.k
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.