Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kibiti (KUU) , wakiongozwa na Mwenyekiti Kanali Joseph Kolombo imefanya ziara ya kutembelea Visima 5 vya maji kati ya 900 kwa nchi nzima vilivyotolewa fedha na , Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye amedhamiria kwa dhati kumtua mama ndogo kichwani.
Kwa nyakati tofauti wakiwa katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya Kanali Kolombo ameridhishwa na mwenendo wa utekelezaji wa mradi huo baada ya kujionea maji yakitoka katika visima vyote huku akisisitiza kuwa siyo visima vya kukauka vimechimbwa kitaalam.
Akitoa pongezi kwa Mhe. Rais Kanali Kolombo ametoa rai kwa wakazi waliofikiwa na mradi huo, kuhakikisha wanalinda na kutunza vizuri visima hivyo ili vikaweze kutumika kwa muda mrefu sambamba na kutunza miundombinu ya visima hivyo ( mabomba , Sola nk.)
Vilevile Kanali Kolombo amewapongeza na kuwashukuru wananchi wote waliowiwa kutoa maeneo yao kwa ajili ya mradi huo wa uchimbaji wa visima ambao kwa sasa unanufaisha wakazi wengi na kupumzika kwenda mbali kutafuta maji.
Hata hivyo, Kanali Kolombo amemwagiza Meneja wa RUWASA kuhakikisha kabla ya kukabidhi mradi huo, visima vyote viwe vimeandikwa kuwa ni visima vya Mama ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya vizazi vijavyo.
Kwa upande wao wananchi wamemshukuru sana Mhe. Rais kwa kwa kuwakumbuka katika huduma hiyo muhimu, na wameahidi kulinda visima hivyo pamoja na miundombinu yake. Wananchi hao pia wameomba maeneo ya mradi kuwekewa taa, huku wakiomba panapomajakiwa visima hi yo viongezwe katika maeneo mengine kwani Bado changamoto ipo.
Aidha licha ya kushukuru Serikali ya awamu ya sita Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kibiti Ndg. Ramadhan Mabula amesema miradi imetekelezwa katika Kata ya Mchukwi Kijiji cha mangwi, Nyakaumbanga, Kata ya Ruaruke Kijiji cha Nyamatanga, Rungungu, na Kata ya Bungu (Pagae).
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.