Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali.Joseph Kolombo mapema hii leo tarehe 9/12/2024 amewaongoza Wananchi wa Kibiti katika zoezi la kufanya Usafi kama sehemu ya kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania.
Zoezi hilo limefanyika katika sehemu mbalimbali ikiwemo maeneo ya Kituo cha Mabasi Kibiti, maeneo yanayolizunguka Soko la Kibiti pamoja na kando kando ya Barabara kuu inayopita kuelekea Mikoa ya Lindi na Mtwara.
Akizungumza wakati wa Zoezi hilo Kanali Kolombo amewataka wamiliki wa baadhi vyumba vya biashara vinavyolizunguka Soko la Kibiti ambavyo vingi bado havijakamilika kukumbuka kufanya usafi mara kwa mara kwa ajili ya kuweka safi mazingira yanayoyazunguka maeneo hayo.
‘’Leo tumeshiriki zoezi la kufanya usafi ikiwa ni sehemu ya maagizo yaliyotolewa na Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuadhimisha Siku hii ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa ngazi ya Wilaya,tumefanya usafi katika soko hili lakini bado siridhishwi na hali ya Usafi katika eneo hili.Wako baadhi ya watu ambao wamechukua vyumba vya biashara na kuvijenga nusu na wameondoka wameacha maeneo hayo yakiendelea kuota nyasi’’
Katika hatua nyingine amewataka Viongozi wa Serikali za Mitaa Pamoja na Viongozi wa Soko la Kibiti kuhakikisha swala la usafi linafwatiliwa na kuwawajibisha wale ambao watakiuka misingi hiyo ikiwemo kutozwa faini na Shilingi 50000 kwa kushindwa kutimiza agizo hilo.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.