KIBITI YAKABIDHIWA BOTI NA WWF TANZANIA
Tarehe 11 Oktoba,2021 kulifanyika hafla fupi kwa WWF Tanzania kukabidhi Boti ya doria yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni miamoja na hamsini kwa uongozi wa Wilaya ya Kibiti.
Boti hiyo kubwa yenye injini mbili zenye nguvu ya Farasi(150HP) kila moja imekabidhiwa kwa mkuu wa Wilaya ya Kibiti Mhe.Kanali Ahmed Abbasi Ahmed aliyeambatana na mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibiti Mhe.Ramadhani Shaha Mpendu pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri Bw.Mohamed i. Mavura.
Pamoja na mazungumzo mengine yakuboresha ushirikiano Mhe. Mkuu wa Wilaya amewashukuru WWF kwa kuwapatia Boti hiyo kubwa itakayosaidia katika ulinzi na usimamizi wa rasilimali zinazotokana na uvuvi na Mikoko.
Katika hafla hiyo ambayo ilifanyika ofisi za WWF zilizoko Mikocheni Jijini Dar es salaam pia ilihudhuriwa na Bw.Mathayo Werema ambae ni Kaimu Afisa Mfawidhi wa Ulinzi wa Rasilimali za uvuvi-Kanda ya Bahari ya Hindi na Kaskazini Mashariki akimwakilisha Mkurugenzi wa Uvuvi aliwasilisha maelekezo ya Mkurugenzi wa uvuvi,kwa kuwashukuru WWF kwa kuunga mkono juhudi za Serikali juu ya Ulinzi wa Rasilimali za Uvuvi na Mikoko na kuomba uongozi wa Wilaya ya Kibiti kuitunza Boti hiyo vema ili adhma ya ulinzi na Usimamizi wa Rasilimali za uvuvi ifikiwe kikamilifu.
Aidha,Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Ramadhani Sasha Mpendu alitoa neno la shukrani na kuwaomba WWF wasiishie kwenye Boti kama watakuwa na fursa zingine wasisite kuwasaidia kwani Kibiti bado ni changa inahitaji sana kusaidiwa ili iweze kusonga mbele .
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.