Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri Wilaya ya Kibiti, Kanali Joseph Kolombo ameendesha kikao cha kawaida cha kamati ya ushauri (DCC) kilichofanyika leo 10.8.2023 katika ukumbi wa Halmashauri ambapo ajenda zote zimepitishwa.
Katika kikao hicho Mwenyekiti kanali Kolombo amewaelekeza Wajumbe, kuendelea kufuatilia na kutekeleza ajenda ambazo hazijafanyiwa kazi na kuzikamilisha kwa wakati ili ziweze kuwasilishwa katika kikao kijacho.
Akiongelea kuhusu ombi la kubadilishwa kwa jina la delta ya Rufiji na kuwa delta ya Kibiti Kanali kolombo amesema amelipokea atalifanyia kazi kwa kuliwasilisha ombi hilo katika ngazi za juu.
Katika kikao hicho taarifa zilizowasilishwa ni pamoja na kupokea taarifa za utendaji kazi za Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kuanzia mwezi January 2023 mpaka Juni 2023 kupitia idara mbalimbali, taarifa za Taasisi za Tanesco na REA, Wakala wa Misitu TFS, TARURA, NMB, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) sekta ya maji RUWASA n.k
Aidha, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kibiti Juma Ndaruke amesisitiza Wajumbe kutekeleza makubaliano ya kikao kwa haraka ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa katika masuala ya msingi.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji na Katibu wa kikao Bw. Hemed Magaro amesema, changamoto, maoni, maelekezo na maboresho yote ameyapokea na kuahidi kuyafanyia kazi kwa wakati.
Kikao hicho kimeudhuriwa na Kamati ya ulinzi na usalama, Wakuu wa Idara na vitengo, Madiwani, Watendaji Kata,Viongozi wa Dini ,Chama na Taasisi mbalimbali.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.