Msimu mpya wa Mauzo ya korosho katika Halmashauri ya Wilaya ya kibiti umezinduliwa rasmi katika ukumbi wa Halmashauri hiyo, ikiwa ni utaratibu wa kawaida kwa Wadau wa korosho kukutana na kujadili ili kuboresha taratibu mbalimbali za uuzaji wa zao la Korosho kwa msimu husika.
Akizindua mkutano huo mkuu wa wilaya ya Rufiji anaekaimu Wilaya ya Kibiti Meja Edward Gowele amewapongeza wakulima na Uongozi mzima wa Wilaya ya kibiti kwa kuibuka kinara wa usimamizi bora wa zao la korosho dhidi ya Wilaya zote za Mkoa Pwani.
Meja Gowele amesema kwa mwaka huu mfumo wa stakabadhi ghalani ndiyo utakaotumika katika manunuzi ya korosho katika wilaya ya kibiti hivyo amewataka maafisa ugani kuhakikisha wanasimamia mfumo huo unatumika.
Vilevile Mkuu wa Wilaya Gowele akavitaka Vyama vya msingi kuhakikisha havipokei korosho ambazo hazijachambuliwa na kuwekwa kwenye madaraja ili kupokea korosho zenye viwango. pia, ametoa angalizo kwa watoroshaji wa korosho kuacha mara moja kitendo hicho ,kwani serikali imejipanga na atakayekamatwa hapatakua na mjadala hivyo akatoa agizo kwa kamati ya ulinzi na usalama na mkurugenzi mtendaji kusimamia hilo kikamilifu.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Mohamed Mavura katika uzinduzi huo akimkaribisha mgeni rasm ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo amewapongeza wakulima na amsema zao la korosho ni uti wa mgongo wa mapato ya wilaya ya kibiti ambapo mwaka huu wilaya ya kibiti imeuza jumla ya kg 7,601,539.
Mwisho wadau wakakubaliana na ombi la Mkurugenzi kuhusu kurejesha tozo ya Tsh. 20 katika kila kilo ya korosho ambayo awali iliondolewa baada ya kuonekana imekuwa mzigo kwa wakulima kutokana na uzalishaji kuwa chini ili kulinda maslahi ya Wakulima kwani makusanyo hayo ya fedha husaidia kuchangia maendeleo ya elimu hususani ujenzi wa vyoo, ukamilishaji wa maboma n.k.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.