Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti imeupongeza umoja wa wanafunzi waliohitimu Msafiri Sekondari arimaarufu ALUMNI Msafiri kwa kuandaa Kongamano lenye tija kwa jamii waliyotoka na kuwasihi iwe endelevu kwa maendeleo ya mtoto wa Kibiti ..
Katika Kongamano hilo wahitimu hao wa Msafiri Sekondari na waandaaji wa kongamano wametoa zawadi ya mashine ya kudurufu (Photocopy machine) yenye thamani ya shiilingi za kitanzania 800,000.ikiwa ni sehemu ya kuikumbuka na kuijali shule waliyosoma.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika Kongamano hilo Anna Shitindi ambaye ni Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Kibiti amesema Kongamano hilo ni la kuigwa na ni chachu ya maendeleo ya Elimu Katika Wilaya ya Kibiti Pia amewashukuru Alumni hao kwa zawadi mbalimbali walizoleta ikiwemo mashine ya kudurufu na kuutaka uongozi wa shule wajielekeze kwenye matumizi sahihi ya mashine hiyo ili kuitunza na kudumunayo kwa muda mrefu.
Akijibu maombi ya Alumni hao kwa kupita risala yao ambapo waliiomba serikali kuweka angalau vyuo vya ufundi na ngazi ya kati (collage) katika Wilaya ya Kibiti Ili kusaidia vijana ambao hawakufaulu vizuri kujiendeleza kielimu akasema amelipokea na litafanyiwa kazi, hata hivyo Kuna mpango kabambe wa kuhakikisha Wilaya inaongeza shule za kidato Cha 5 na 6 zifike angalau 3 Ili kuipunguzia mzigo kibiti Sekondari ambayo ni shule pekee wilayani.
Vilevile Bi Shitindi kwa niaba ya Mkurugenzi ambaye alikuwa Mgeni Rasmi amewasihi wazazi kuwaandikisha mapema watoto watoto waliofikia umri wa kuanza darasa la awali na la kwanza Ili January ikifika wawe wamekwisha waandalia mahitaji muhimu Kwani serikali huwasomesha watoto bila ada hivyo wasisite kuandikisha watoto .
Pia akasema anasikitishwa na tabia za mmomonyoko wa maadili zinazoendelea kwa watoto ikiwa ni pamoja na utoro shuleni, mimba n.k maadili yakisimamiwa vizuri na wazazi huku walimu hawatapata shida itasaidia pia kauli mbiu ya Wilaya ya Tokomeza ziro pandisha GPA.
Aidhaa Afisa Elimu huyo amesema, Kuna haja ya kuelekeza nguvu ya changizo la chakula katika Kongamano lijalo kwani chakula ni afya, hivyo atafurahi kuona chakula shuleni kwani chakula huleta mahusiano mazuri ya kitaaluma .
Mwisho kipekee akampongeza Mwenyekiti wa uvccm Wilaya ya Kibiti ambaye ni mmoja wa wahitimu wa kwanza 2010 Bi Amina Mkomboya kwa zawadi nzuri za taulo za kike za kuwasitiri watoto wa kike yaan Pedi ambazo ziligawiwa kwa mabinti hao.
Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo Estomic Kimwemwe amesema Kongamano hilo ni mwendelezo kwa ushirikiano mzuri wa wanafunzi waliohitimu Msafiri Sekondari ambalo hufanyika Kila mwaka kwa njia ya kuchangishana wao kwa wao na kuja kurudisha shukrani shuleni kwapo huku lengo likiwa kuhamasisha wadogo zao kusoma kwa bidii...
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.