Kama ilivyo desturi ya nchi yetu kila ifikiapo Julai 25 ya kila Mwaka, Tanzania huadhimisha siku ya kuwakumbuka mashujaa wa Tanzania waliojitolea maisha yao kwa ajili kuutetea, kuupigania na kuulinda Uhuru wa nchi yetu.
Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti imeungana na Watanzania wote katika siku hii ya leo kukumbuka mema yaliyofanywa na mashujaa hao kwa kufanya shughuli ya kijamii ya Usafi katika kituo cha Afya Kibiti pamoja na kuwaombea Dua na Sala fupi mashujaa wetu na kuiombea Amani Nchi yetu kutoka kwa Viongozi wa Dini.
Misingi mizuri na imara iliyojengwa na mashujaa hao pamoja na wasisi wa Taifa letu baba wa Taifa, Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume, bado tunaiishi kwakuwa imesababisha Wananchi wa Tanzania tukiwemo Kibiti kwa muda mrefu kuishi kwa Amani na Utulivu, huku tukifanya mambo yetu kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu yeyote.
Shughuli hii imehudhuriwa na Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Vyama, Wahe. Madiwani, Viongozi wa dini, Watumishi wa Serikali, Taasisi za Umma, Taasisi Binafsi pamoja na Wananchi wa Kibiti.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.