4.6.2024
Hatimaye ni zamu ya Kibiti, Jopo la madaktari bingwa wa Rais SSH wa magonjwa mbalimbali limewasili wilayani Kibiti kwa siku 7 kwa lengo la kutoa huduma za magonjwa mbalimbali kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na kutoa rufaa kwa wale watakaohitajika kupewa.
Madaktari waliowasili ni Daktari bingwa wa huduma ya ganzi na usingizi, Daktari bingwa wa huduma ya magonjwa ya watoto na watoto wachanga (pediatric), Daktari bingwa wa huduma ya magonjwa ya ndani (shinikizo la damu, kusukari, Figo n.k), Daktari bingwa wa huduma ya magonjwa ya uzazi, wajawazito na Wanawake (gynecology) na Daktari bingwa wa huduma ya upasuaji (mabusha, kidole tumbo, uvimbe mkubwa na mdogo, mifupa na magonjwa ya mifupa).
Akiwapokea madaktari hao Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo amewashukuru madaktari hao kwa kufika akisema ni imani yake kwamba wananchi wa Kibiti wenye matatizo ya kiafya watapata huduma. Pia amewataka wananchi wote wa Kibiti wenye kuhitaji matibabu kujitokeza kwa wingi katika hospitali wa Wilaya (Upazi) kupatiwa matibabu.
Aidha, Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Elizabeth Oming'o amesema kupitia ugeni huo wamejipanga vizuri kushirikiana na madaktari hao kuhakikisha wateja wote wenye changamoto za matibabu yanayotolewa wanahudumiwa ipaswavyo.
Kwa habari picha ni matukio madaktari wakiwahudimia wananchi wa Kibiti.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.