Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imeendesha mafunzo ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa Wahe. Madiwani na Wakuu wa Idara Wilayani Kibiti jana tarehe 13 Juni, 2024.
Lengo la mafunzo hayo ni kuwakumbusha na kuwaelekeza Viongozi hao (Wazoefu na Wapya) taratibu, Sheria na Miongozo ya kufuata wanapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Sambamba na mafunzo hayo Viongozi watatu (03) ambao ni wapya walitoa tamko la Uadilifu mbele ya wajumbe wa Sekretarieti ya Maadili pamoja na Viongozi wenzao kama sheria inavyowataka kwakuwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ndiyo inayosimamia jukumu hilo.
Viongozi hao waliotoa tamko la Uadilifu ni: Diwani wa Kata ya Mahege Mhe. Hamada Hingi, Diwani wa Kata ya Mlanzi Mhe. Athumani Mketo pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Ugavi na Manunuzi Bi. Yohana Thomas.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.