12.06.2024.
Ikiwa ni msimu mwingine tena, Taasisi ya Mama ongea na Mwanao kupitia Kampuni yake ya mama SAMIA NIVISHE VIATU imeanza zoezi la kuvisha viatu Mkoa wa Pwani katika shule ya Msingi Kitundu yenye kituo cha wanafunzi wenye mahitaji maalum ambapo wamemkabidhi Mkuu wa Wilaya hiyo jozi 150 za viatu na baiskeli 10 (wheelchair) kwa ajili ya watoto wenye uhitaji maalum.
Kabla ya kukabidhi msaada huo Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Ndg. Steve Mengele amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kibiti kwa kuacha kazi zake na kuungana nao katika zoezi hilo.
Akipokea msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo sambamba na Viongozi wengine ametoa shukrani zake za dhati kwa Taasisi hiyo Mama Samia huku akikiri wazi kuwa Rais wetu ni mama wa watoto wote.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Ndg. Hemed S. Magaro ameipongeza Taasisi hiyo kwa ubunifu wa kipekee, kwani wazo lao linawafikia watoto wengi ukizingatia bado uhitaji ni mkubwa katika jamii zinazowazunguka.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.