Katika kuhakikisha tunakwenda sambamba na Teknolojia Nchini Naibu wa Waziri , Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira khamis Hamza Khamis (MB), amewaagiza walimu kuhakikisha wanaongeza juhudi za ufundishaji wa masomo ya sayansi ili kuzalisha kizazi chenye wataalam watakaoipeleka nchi Dunia inakoelekea, huku akiwasisitiza Wazazi kuwasimamia watoto wao
Amesema hayo Oktoba 10 alipokuwa akifungua jengo la Ofisi ya rasilimsli katika Kijiji cha Nyamisati Wilayani Kibiti lililojengwa na shirika la Uhifadhi wa Ardhi Oevu (Wetlands International).
Licha ya kupanda mikoko takribani 500 Wilayani humo, Mhe. Khamis ameiagiza Halmashauri na Wetlands kudhibiti ongezeko la uingiaji wa maji chumvi kwenye mito kwani imekuwa ni chanzo cha uharibifu wa vipando vya mikoko vinavyoendelea kupandwa.
Hata hivyo ametoa wito kwa wakazi wa kibiti na watanzania kwa ujumla kuongeza kasi ya kupanda mikoko na miti ya kawaida, kuepuka kufanya shughuli za kibinadanu kwenye vyanzo vya maji,na pia kusimamia Sheria za utunzaji wa mazingira.
" Halmashauri simamieni uthibiti shughuli za kibinadamu katika maeneo ya vyanzo asilia,ili kuimarisha utunzaji w Mazingira kwenye maeneo yenu" Alisema.
Akimwakilisha Mkuu w Wilaya ya Kibiti, Afisa Tarafa ya Kikale Ndugu. Salim Malogwa amemshukuru Mhe. Khamis Hamza Khamis kwa kuitikia wito pamoja na kuwapongeza Wetlands kwa kuwa nguzo kubwa ya uhifadhi na urejeshaji wa uoto wa asili Kibiti.
Kwa upande wake Mratibu wetland International Tanzania Dkt. Emanuel Mwainunu amesema kuzinduluwa kwa jengo hilo, litatumika kama Ofisi ya Wetlands na Taasisi zingine, litakuwa Kituo cha kutoa elimu ya rasilimali ya matumizi endelevu ya uwanda wa delta ya Rufiji, kuwa Kituo cha wanafunzi kufanya utafiti na kutoa taarifa,n.k
Aidha Diwani wa Kata ya Salale Mhe. Abdallah Ndomondo na Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Kibiti Mhe. Twaha Mpembenwe amelipongeza shirika hilo kwa kazi nzuri wanavyofanya ya kutunza Mazingira na wakati huo huo Diwani wa Kata ya Kiongoroni Mhe. Mharami Tota alimshukuru Mhe. Rais kwa kuwapatia kibali cha kutekeleza Mipango hiyo yote kwa maelekezo yake.
Awali akifungua hafla
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.