MKACHAPE KAZI SIYO KUKAA OFISINI.
KILA MMOJA AWAJIBIKE KUTIMIZA MAJUMU YAKE.
Afisa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Kibiti Bwenda Ismail Bainga amewaagiza watumishi wa idara hiyo kutekeleza majukumu yao kwa kuwajibika ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuifikia jamii kuanzia ngazi ya Kitongoji mpaka Wilaya na siyo kukaa ofisini pekee.
Hayo yamejiri katika kikao kazi kilichobeba ajenda zenye mikakati ya kuimarisha utendaji kazi ndani ya Idara wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo ambapo Bainga amewaagiza watumishi wote wa kuhakikisha kila mmoja anawajibika kwa upande wake kwa kufuata kanuni na taratibu za maelekezo ya kazi kwani hatokuwa tayari kumvumilia mtumishi ambaye hawajibiki.
Kwa upande wa kilimo ,Bainga amewaagiza Maafisa kilimo wote kuhakikisha wanasimamia na kuelekeza wakulima juu ya kilimo Bora na cha kisasa kwenye zao la korosho,ufuta na mazao mengine ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri sahihi wa kilimo kulingana na majira ya msimu. Katika hatua hiyo wamekubaliana Maafisa kilimo wote kuwa na mashamba darasa 10 na kuhakikisha kila mwezi Mtumishi anawafikia wakulima 50 -100 .
Vilevile Bainga amewataka viongozi hao kuhakikisha wakulima wanafanya usaili kwa ajili ya pembejeo za ruzuku kama ilivyoekezwa wakati wakiwa katika mkakati wa kupata wakala mwenye uwezo wa kukidhi zoezi la usambazaji wa mbolea,pia kusimamia ujazaji wa fomu Kwa usahihi ili kuwasilisha Kwa wakati taarifa za ARDS kuonyesha hekari sahihi zilizotumika na mwisho wa kujaza fomu hizo ni tarehe 5 ya Kila Mwezi .
Vilevile Mkuu huyo wa Idara ya Mifugo amewaagiza Maafisa mifugo wote kusimamia uundwaji wa kamati za maridhiano zitakazokuwa zinasaidia kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji kuanzia ngazi za chini, kuhakikisha wafugaji wote wameorodhesha kwa usahihi idadi ya mifugo wanayoimiliki na kusimamia utekelezaji wa minada .
Hata hivyo amesisitiza utoaji wa elimu ya umuhimu wa uwepo wa Ranchi ili kila mwenye uwezo wa kuanzisha Ranchi awasilishe maombi kwa Mtendaji wa kijiji kwani utaratibu wa kugawa maeneo hayo unaendelea na mwisho wa Kupokea majina ni 30/1/2023 ambapo mpaka Sasa Kata ya Mtunda imeshaanzisha Ranchi sambamba na kufanya kampeni za kutoa elimu ya milipuko ya magonjwa ya mifugo kama vile NDIGANA ambao huhatarisha uhai wa mifugo kwa muda mfupi.katika hatua nyingine wamejiwekea mpango kazi wa uhamasishaji na kuwafikia wafugaji 20 kwa mwezi na kuwa na wafugaji wasiopungua 3 watatu kwa ajili ya shamba darasa.
Aidha ameielekeza idara ya Uvuvi kuanzisha mabwawa mapya ya ufugaji wa samaki ambayo yatakuwa ya mfano kwa waliotayari kuanzisha na kutoa elimu ya ufugaji huo huku akisisitiza kukusanya wa mapato kikamilifu kwa kuwatumia BMU katika maeneo yote ya uvuvi.Katika kipengele hicho wameweka mikakati ya kila afisa uvuvi kuanzisha mabwawa 2 na kuhakikisha wanawafikia wavuvi 15 kwa mwezi lengo likiwa ni kuifikia jamii kila kona kujali Mazingira ya eneo husika katika kuhakikisha huduma zinawafikia walengwa huku akisisitiza kuwa na Vyama vya ushirika imara vinavyofanya kazi vizuri.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.