MKURABITA YAENDESHA MAFUNZO KWA WAKULIMA KIBITI JUU YA UTUMIAJI WA HATI ZA KIMILA KIUCHUMI.
Wakulima wa Vijiji vya Jaribu Mpakani na Mchukwi ‘A’ wapatiwa mafunzo juu ya utumiaji wa Hati za Kimila katika shughuli za kiuchumi kwani Vijiji hivi teyari vina mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Mafunzo haya muhimu kwa jamii yalitolewa na MKURABITA ambapo mada zilizotolewa ilikuwa ni utunzaji wa kumbukumbu za mahesabu ya kilimo,Kilimo biashara,Kanuni bora za kilimo,Utafutaji wa fursa na namna ya kuzitumia,Mpango wa biashara na Uthamini na utunzaji wa mazingira .
Mafunzo haya muhimu yameweza kuwafungua macho jamii na kutambua fursa mbalimbali zinazoweza kupatika na hati hizi pia wameweza kutambua thamani ya ardhi.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.