Leo tarehe 19.10.2023, Mwenyekiti wa masuala ya Lishe wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo amefungua kikao cha tathmini ya mkataba wa lishe ngazi ya kata kwa robo ya kwanza mwezi Julai-Septemba 2023/2024 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Katika ufunguzi huo Kanali Kolombo amesema katika kuhakikisha afya za watoto zinaimarika ni lazma kuwe na zoezi la ufuatiliaji endelevu kuanzia mtoto anapozaliwa mpaka anapofikisha miaka mitano.
Katibu masuala ya Lishe Wilaya ya Kibiti Bw. Hemed Magaro amesema agenda ya Lishe wilayani iwe ni ya lazima na kuona umuhimu wa kutoka elimu kwa wananchi, kuwasimamia na kuhakikisha kila kaya inakuwa na hekari 2-3 za chakula.
Vilevile Bw. Magaro amewaelekeza watendaji kusimami na kuhakikisha mashamba ya shule yanalimwa kwa tija na kuyatunza vizuri sambamba na kufanya kampeni ya kupita shule kwa shule kuhamasisha kilimo cha chakula na mbogamboga Shuleni.
Vilevile katika kikao hicho Katibu Tawala wa Wilaya Bi Mariam Katemana ameshauri kuwa kutumia WAVI (wahudumu wa Afya wa vijiji) pamojana kuwatengea bajeti ya kuwasapoti kuweza kutoa elimu ya kaya kwa kaya wanapokuwa na ajenda ya kupita katika kaya hizo wakati wa shughulu zao za kila siku.
Hata hivyo Bi Katemana amesema katika msimu huu wa kilimo, ni muhimu kuwaandikia wakuu wa shule barua ili kusisitiza suala la kilimo mashuleni, jambo litakalowasaidia kupata chakula na chanzo cha mapato shuleni.
Akisoma taarifa ya Lishe Wilaya Afisa Lishe Bi. Roina Daza amesema katika kikao kilichopita waliadhimia kuwasaidia Watoto wenye hali mbaya ya lishe ambapo jumla ya sh. 521,850 zilipele kwa Watoto 6 wa familia 3 tofauti zenye watoto wenye lishe duni (Utapiamlo) kwa kuwanunulia chakula na kuwekewa bili ya maziwa, ikiwa ni michango ya wananchi mbalimbali wa Halmashauri hiyo. Kati ya Watoto hao walikuwepo mapacha 3 wa miezi minne kutoka Kata ya Dimani, Mapacha 2 wa miaka 2 na nusu kutoka Kijiji cha Mangombela kata ya Bungu,na mtoto wa miaka 5 wa Bungu.
" Tumekuwa na taarifa za watoto mapacha wenye afya duni, habari njema ni kwamba baada ya msaada huo, sasa mmoja wa pacha hao wa miaka miwili sasa ameanza kutembea" Alisema Daza.
Bi. Daza amefafanua kuwa kikao kilichopita waliagizwa kupitia na kujua takwimu ya idadi ya shule na watoto wanaopata chakula shuleni, watendaji kata kuhakikisha ajenda ya Lishe inakuwaya kudumu, kufuatilia familia zenye ya utapiamlo, kutoa elimu ya uzazi wa mpango, kusimamia shule zotekuwana mashamba darasa na kuhamasisha wazazi zoezi la uchangiaji wa chakula n.k
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.