MKUU WA WILAYA KIBITI AFUNGUA MNADA WA KWANZA WA UUZAJI WA KOROSHO MKOA WA PWANI.
Leo tarehe 20-10-2021asubuhi mkuu wa Wilaya Kibiti Mhe.Kanali Ahmed Abbas Ahmed amefungua mnada wa kwanza wa korosho katika Mkoa wa Pwani kwa msimu wa mwaka 2021 uliofanyika Wilayani Kibiti ambapo jumla ya tani 3,087,901 ziliuzwa.
Katika mnada huo Wilaya ya Kibiti iliuza jumla ya tani 1.808.769 ikiwa ni zaidi ya nusu ya mzigo uliouzwa leo.Jumla ya makampuni 12 yalijitokeza kununua korosho hizi.Koroho daraja la “A” zimeuzwa shilingi 1,951.48 na daraja “B” shilingi 1,600.62.
Kwenye mnada huo wakulima walifazaishwa sana na bei ya korosho kuwa chini hali ya kuwa korosho zao zina ubora uliokidhi viwango.kitu ambacho kinawakatika tama ya kuendelea kulima zao hili kwani ni mwaka wa tatu wakulima hao wameuza korosho zao kwa hasara.
Mhe.mkuu wa Wilaya amelipokea suala lao kwa masikitiko makubwa na kuahidi kulifanyia kazi suala hili katika msimu ujao wa mavuno na pia aliwaasa wakulima wasikate tamaa.
Aidha,Leo mchana Mhe.Mkuu wa Wilaya alifanya mkutano wa hadhara na Wananchi wa Kata ya Kibiti kusikiliza kero zao na kuhimiza maendeleo.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.