Ikiwa ni Mwendelezo wa ziara za ukaguzi wa miradi ya Maendeleo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Ndg. Mohamed I. Mavura akiambatana na maafisa mbalimbali wa serikali wilayani humo wametembelea miradi ya shule za sekondari yenye thamani ya Sh. 420,000,000/= fedha kutoka Serikali Kuu. Fedha hizi zinajenga jumla vyumba 21 vya madarasa katika Kata za Dimani, Mtawanya Bungu na Mwambao.
Akiwa katika shule ya Sekondari Dimani Mavura akakagua eneo ambalo darasa moja litajengwa na kiasi cha shilingi 20,000,000 kimetengwa kwa ajili ya ujenzi huo. Mpaka leo tarehe 19/10/2022 mafundi wamekwisha patikana na zoezi la kuchimba msingi linaanza.
Akiwa katika shule ya sekondari ya Mtawanya ambapo kiasi cha sh. 180,000,000/= kimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 9 vya madarasa na ofisi ya walimu, Mkurugenzi amezindua zoezi la ujenzi wa msingi kwa kushiriki katika uchanganyaji saruji na kokoto ili kuamsha hari ya mafundi.
Katika Shule ya Sekondari Nyambili Nyambunda ambapo ujenzi wa vyumba 5 vya madarasa wenye thamani ya sh.100,000,000, Mkurugenzi na Maafisa alioambatana nao wamefurahishwa sana na jitihada za wananchi jinsi walivyo jitokeza kwa wingi kujitolea nguvu zao ii kuhakikisha kwamba ujenzi unakamilika kwa haraka. Hali hii inaonyesha kwamba wananchi wanashauku kubwa kuona Watoto wao wanapata elimu katika eneo la karibu na makazi yao.
Ziara ikahitimishwa katika shule ya Sekondari Mwambao ambapo vyumba 6 vya madarasa vyenye thamani ya sh. 120,000,000. Viongozi wakaridhishwa na hatua za awali kwa zoezi la kuchimba msingi wa boma unaoendelea shuleni hapo.
Katika ziara hiyo kwa nyakati tofauti Mavura ametoa maagizo yafuatayo:
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.