Miradi iliyomulikwa na Mwenge wa uhuru 2023 katika Halmashauri ya Wilaya ya kibiti ni Jengo jipya la Upasuaji katika kituo cha Afya Kibiti, ujenzi wa vyumba 5 vya madarasa na ofisi Moja ya walimu , Klabu ya kuzuia Rushwa chini ya Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa katika shule ya Sekondari Nyambili Nyambunda, Mradi wa kikundi cha vijana cha CAMA Mahege na ujenzi wa daraja la Mkelele.
Licha ya miradi hiyo pia Mwenge wa Uhuru umemulika mradi wa Mazingira katika Kata ya Salale, Mradi wa maji Mahege, Mradi wa ujenzi wa darasa moja na ofisi katika shule ya msingi Roja, ujenzi wa Nyumba ya kulala wageni ya kisasa kabisa katika Kata ya Kibiti.
Miradi mingine iliyomulikwa Mei 21 ni pamoja na mradi wa lishe, Ukimwi, rushwa, Madawa ya kulevya, utunzanji wa mazingira na Ziro Malaria.
Katika sherehe hizo za Mwenge Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kibiti Mhe. Juma Ndaruke ameishukuru timu ya wakimbiza mwenge kwa kuridhika na miradi yote. Pia amewashukuru Viongozi wote wa Wilaya ambao wamepambana kusimamia miradi na kuhakikisha inakamilika. licha ya pongezi ameahidi kushirikiana na Uongozi wa Wilaya kuhakikisha miradi inayoendelea kutekelezwa inakamilika kwa wakati na viwango vy juu.
Naye Mbunge wa Jimbo la kibiti Mhe. Twaha Mpembenwe amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa namna anavyowezesha miradi ya Maendeleo, pia akiwashukuru Viongozi wote wa Wilaya kwa usimamizi mzuri wa Miradi inayoanzishwa, kukamilishiwa na kuendelezwa.
" Niko pamoja nanyi Viongozi na wananchi wangu, ndiyo maana nimeacha shughuli za bunge ili nije kushirikiana nanyi kukimbiza Mwenge wa Uhuru Wilayani kwetu, ambao umezindua, kufungua na kuweka mawe ya mshingi katika miradi yetu, hongereni sana na mtambue Mbunge wenu niko kazini kuwawakilisha vema Bungeni" Alisema Mhe. Mpembenwe.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.