Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo amekabidhiwa Mwenge wa Uhuru kutokea katika Wilaya ya Rufiji Tarehe 06,Aprili,2024 na kisha kuendelea na mbio hizo za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Kibiti.
Mara baada ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru katika eneo la Mkupuka katika Wilaya ya Kibiti Mwenge huo umekimbizwa umbali wa kilomita 119.8 huku ukitembelea, kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye jumla ya miradi 13 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi milioni 610.1.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.