Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam imekabidhi msaada wa mabati 120 yenye thamani ya zaidi ya sh Mil 4 kwa ajili ya kuezeka shule ya Msingi kiasi iliyopo Wilayani Kibiti ambayo iliezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mwaka 2022.
Akikabidhi mabati hayo Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam Ndg. Dismas Prosper amesema, msaada huo ni sehemu ya utaratibu wa benki yao kurudisha shukrani kwenye jamii kwa kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na majanga.
Aliendelea kusema kuwa, NMB ni benki ambayo imejikita kwenye kutatua changamoto zinapotokea lengo likiwa kuhakikisha uwepo wa huduma Bora katika Sekta zote ikiwemo Elimu. Pia amesema wataendelea kuwa wadau wakubwa wa maendeleo ya elimu nchini kwenye masuala mbalimbali na sio yanayohusu majanga pekee.
Katika mapokezi hayo Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo ameishukuru benki ya NMB na Viongozi wake wote kwa kuona umuhimu wa kuwa na utaratibu mzuri wa kurudisha shukrani kwa Jamii jambo linalofanya benki hiyo kuwa karibu zaidi na jamii inayowazunguka.
Kanali Kolombo ameshukuru sana kwa msaada huo huku akikiri kuwa Wilaya ya Kibiti bado inauhitaji mkubwa wa mabati kwani miundombinu mingi ni ya zamani inauhitaji wa ukarabati na katika majenzi mapya yanayoendelea.
"Naomba peleka salam kwa viongozi wenu, tunashukuru sana kwa kutukumbuka na kutujali wanakibiti msichoke kutuunga mkono tukija wakati mwingine. Leo nimepokea mabati haya, niwahakikishie hakuna kipande cha bati kitakachopotea" Alisema Kolombo.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.