22.4.2024
Wakati zoezi la kupokea misaada likiendelea Wilaya ya Kibiti, Jana Tarehe 22 4.2924 Kanali Joseph Kolombo amepokea msaada wa magodoro 80 na ndoo 100 zenye koki vyote vikiwa na thamani ya sh. 8,000,000 kwa ajili ya waathirika wa mafuriko wilayani Kibiti kutoka shirika lisilo la kiserikali la PASSADA linojishuhulisha na kutoa misaada mbalimbali nchini.
Meneja wa shirika la PASSADA Ndg. Cayus Mrina amesema Taasisi yao ni mdau mkubwa wa kutoa huduma Kibiti, hivyo wameguswa kuikimbilia Kibiti kushirikiana pamoja katika janga hili la Mafuriko kwa kuwashika mkono waathirika huku akiushukuru Uongozi wa Wilaya kwa mapokezi mazuri.
Akizungumza kwa niaba ya Askofu Mkuu Mwenyekiti wa Bodi ya PASSADA Padri Christian Likoko amesema kanisa limeona ni vema kuungana na wakazi hao katika kipindi hiki cha dhahama ili kuweza kuwafariji waathirika wa mafuriko.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo amelishukuru shirika hilo la kidini kwa kujitoa kwao kuwasaidia waathirika wa mafuriko Kibiti, kwani msaada waliotoa ni mkubwa na wakipekee sana katika jamii.
Mwisho Kanali Kolombo akipokea msaada huo amewathibitisha PASSADA kuwa atahakikisha walengwa wanafikishiwa msaada huo kama ulivyopokelewa.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.