Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa amewaagiza watumishi wa umma Wilaya ya Kibiti kuwajibika ipasavyo kila mmoja kwa nafasi yake.
Ni katika siku ya pili ya ziara yake mkoa wa Pwani Wilaya ya Kibiti ambapo alizungumza na watumishi katika ukumbi wa Halmashauri hiyo. Vilevile Mhe. Majaliwa amemsimamisha Kazi Afisa maendeleo ya jamii ndg. Godfrey Haule kwa tuhuma za kujihusisha na rushwa Pamoja na kukutwa na sare za jeshi la JWTZ na kutaka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake baada ya uchunguzi wa kamanda wa TAKUKURU kukamilika.
Mbali na kuongea na watumishi Mhe.Waziri Mkuu amepongeza Halmashauri hiyo Kwa kuwa na jengo zuri ambalo lipo katika hatua za umaliziaji baada ya kulikagua.
Mhe. Kassim Majaliwa amewaagiza DC, na DED kusimania uwajibikaji na nidhamu maofisini kwa kuhakikisha watumishi wanafanya kazi Kwa bidii kwa kufuatilia mienendo ya utendaji wao wa kazi,huku akisisitiza kuwa na vikao vya mara kwa mara, Pamoja na kujenga tabia ya kuwatembelea wateja wao(watu wanao wahudumia) hadi maeneo ya vijijini kujua shida zao na siyo kukaa ofisini pekee.
Mhe. Majaliwa ameonyesha kuridhishwa na Halmashauri ya Kibiti kwa kuwa na makusanyo mazuri ya mapato. Hata hivyo pamoja na Kwa na makusanyo mazuri ya mapato,Waziri Mkuu amewataka Mwenyekiti wa Halmashauri na Madiwani kuhakikisha fedha za mapato ya ndani zinatengeneza miradi mkubwa siyo kutegemea Serikali Kuu pekee na kuishirikisha jamii pia .
Kwa upande wa huduma za afya Waziri Mkuu Majaliwa amepongeza jitihada za usimamizi wa jengo la wagonjwa wa dharula (EMD) na kutaka umaliziaji wa milango ufanyike kwa haraka ili kuruhusu huduma kuanza kutolewa haraka. Vile vile amewaagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Mohamed Mavura pamoja na Mwenyekiti Ramadhani Mpendu, kuhakikisha vijiji vyote vinakua na zahanati huku akisema ujenzi wa hospital ya Wilaya ya kibiti ambao upo katika hatua ya umaliziaji ,utapunguza safari ya wananchi kwenda Dar es Salaam kutafuta matibabu kwani ni hospitali ya kisasa yenye huduma zote ikiwa ni pamoja na vipimo vyote muhimu.
Aidha Mhe. Majaliwa ameitaka Halmadhauri ya Kibiti kupitia idara husika,kufungua fursa na kutangaza fursa za vivutio vya utalii vilivyopo katika wilaya hususani katika maeneo ya Delta na mbuga ya selous.
Katika ziara hiyo iliyoambatana na viongozi wa chama na Serikali,Mhe. Mbunge wa Jimbo la Kibiti Twaha Mpembenwe ameipongeza Serikali ya awamu ya 6 Kwa jinsi inavyotoa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo sambamba na kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji Mohamed Mavura Kwa jinsi anavyoshirikiana na Ofisi ya Mbunge kuhakikisha miradi inakamilika Kwa wakati. Pia ameiomba serikali kukamilisha jengo la Halmashauri hiyo ambalo lipo katika hatua ya umaliziaji japo safu ya chini zimeanza kutumika.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.