AHAIDI KUTATUA CHANGAMOTO ZILIZOPO
Waziri wa Elimu sayansi na teknolojia Prof. Adolf Mkenda amefanya ziara ya kutembelea shule ya sekondari ya wasichana Wama na kayama katika Wilaya ya Kibiti.
Akiwa shuleni hapo Prof. Mkenda amesema lengo la ziara hiyo ni kutembelea shule hiyo kuona mafanikio yaliyopo, changamoto na kuangalia namna ya kuzitatua.
"Tunamshukuru mama Salma Kikwete kwa kuona umuhimu wa kuleta shule hii eneo hili ni msaada mkubwa katika jamii inayowazunguka" Alisema Prof Mkenda.
Prof. Mkenda amesema changamoto za miundombinu ya shule ikiwa ni pamoja na ukosefu wa uzio amezibeba na atazifanyia kazi.
Hata hivyo prof Mkenda amemshukuru na amempongeza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kujali maendeleo ya elimu Kwa kuleta fedha nyingi kwa ajili ya majenzi mbalimbali ya vyumba vya madarasa na mikopo ya elimu ya juu.
Pia Waziri Mkenda amewahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii hususani masomo ya sayansi, kwani watakaofaulu vizuri watapata ufadhili wa Serikali kwa 100% (Samia scholarship) kuendelea na masomo ya elimu ya juu.
Akimkaribisha Waziri Wa Elimu Sayansi na Teknologia , Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo amempongeza Waziri kwa kufika Wilaya ya Kibiti huku akiwasisitiza na kuwakaribisha kibiti Kwa ajili ya uwekezaji.
" kibiti ni mahali salama karibuni kwa uwekezaji, tuna maeneo ya kutosha yenye rutuba nzuri kwa kuwekeza".
Awali Akisoma taarifa ya mafanikio ya shule Mwenyekiti Msaidizi Mohamed Zome amesema tangu shule ianzishwe imekuwa na maendeleo mazuri kitaaluma na kufaulisha vizuri .
Hata hivyo amesema licha ya mafanikio pia shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa miundombinu (majengo) upungufu wa nyumba za Walimu, upungufu wa Walimu na kuchelewa kuripoti kwa wanafunzi wa kidato Cha kwanza.
Wamanakayama ni Taasisi ya Wanawake na Maendeleo ambayo husaidia kusomesha watoto yatima na wanaotoka katika mazingira duni Tanzania bara na visiwani ambapo katika Mkoa wa Pwani ni Wana na kayama na Kwa mkoa wa lindi hujulikana kwa jina la Wama Sharaf.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.