WANAWAKE WILAYANI KIBITI WASHEREKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KIVINGINE.
Zikiwa zimesalia siku mbili kuelekea sherehe ya siku ya wanawake duniani, Wanawake Wilayani Kibiti wamefanya usafi kituo cha Afya Kibiti , Pamoja na kuwafariji wagonjwa wa kituo hicho kwa zawadi mbalimbali. Pia wametembelea shule ya sekondari Mjawa ili kutoa motisha kwa wanafunzi wanaofanya vizuri .
Wakiwa katika kituo cha Afya kibiti wamefanya usafi wa mazingira kwa ujumla, kuwafariji wagonjwa katika wodi la Wazazi, Watoto, na wodi la wanaume pamoja na kutoa zawadi mbalimbali kama vile Sabuni za kufulia ,maji ya kunywa , biskuti , juisi na nguo za watoto Kwa watoto 7 wachanga.
Vilevile wametembelea shule ya sekondari Mjawa ambapo walikutana na wasichana wa kidato Cha 1-4 na kutoa zawadi ya madaftari na kalamu kalamu kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye masomo yao na wakiwasihi kusoma kwa bidii. Mbali na zawadi hizo za masomo , wametoa taulo za kike kwa ajili ya wanafunzi wote wa kike shuleni hapo.
Pia wakiwa shuleni hapo walitoa mada mbalimbali zenye hamasa Kwa watoto kuhusu kujitambua, umuhimu wa elimu,kujiepusha na vishawishi n.k.
Maadhimisho hayo yenye kaulimbiu isemayo UBUNIFU NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA NI CHACHU KATIKA KULETA USAWA WA KIJINSIA yanatarajiwa kufanyika kesho 7/3/2023 kiwilaya katika uwanja wa Samora uliyopo nje kidogo ya mji wa Kibiti, wakati katika ngazi ya MKOA yatafanyika wilayani Bagamoyo siku ya kilele Cha sherehe hiyo machi 8.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.