Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) imeanza zoezi la ufuatiliaji wa utekelezaji wa matumizi ya mwalimu msaidizi jamii wa elimu ya awali katika vituo vya utayari vyenye kusudi la kumuandaa mtoto ambaye hajawahi kupata elimu ya awali, kuwa na utayari wa kuanza Darasa la Kwanza mwaka 2023.
Ufuatiliaji huo umelenga kuona jinsi mwalimu anavyoweza kutumia vitabu vya hadithi vinavyowezesha mtoto kuanza darasa la Kwanza na uhalisia ukaonekana Kwa jinsi watoto walivyohadithia hadithi mbalimbali,utambuzi wa namba ,Picha na uimbaji wa nyimbo Kwa umahiri.
Akiwa Wilayani Kibiti Mwesiga Kabigumila ambaye ni Mratibu wa Proramu ya shule Bora Kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) amesema vituo hivyo vimeanzishwa chini ya program ya Shule Bora kwa lengo la kuwapunguzia safari watoto wenye umri mdogo, wasitembee umbali mrefu kuitafuta elimu lakini kumuandaa mtoto kuwa tayari kuanza shule.
Hata hivyo Mratibu Kabigumila ameridhishwa na namna Walimu Wasaidizi Jamii wa walivyotumia zana, njia na mbinu mbalimbali za kuwaaanda watoto kuwa tayari kuanza shule, katika ziara hiyo watoto wameonesha uchangamfu na utayari wa kuanza darasa la kwanza Kwa vitendo kutokana na uelewa walioupata darasani.
Vilevile Kabigumila ambaye pia kitaaluma ni Mwalimu amewapongeza Walimu Wasaidizi wa Jamii kwa kukubali jukumu la kuwaandaa watoto hao katika vituo vyote vya mkoa wa Pwani hususani Kibiti,pia amewapongeza wazazi wote waliokubali watoto wao kuandaliwa katika vituo hivyo huku akiwasisitiza kuhakikisha wanapata eneo la kujenga vyumba vya madarasa ya kusomea.wakati huo huo amewataka wazazi wote kuwaandikisha watoto katika shule mama huku wakiendelea kusoma walipo chini ya uangalizi wa shule mama wakati shule shikizi zikiandaliwa kujengwa .
Awali kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kibiti Mwalimu Violet Mahimbo ambaye ni Afisa Taaluma Msingi,mbele ya Mratibu aliomba watoto waendelee kufundishwa kwa ajiri ya utayari wakati Uongozi wa Wilaya na wakazi wa maeneo husika wanapambana kuhakikisha eneo la ujenzi wa madarasa linapatikana .
Pia mwalimu Mahimbo amefurahishwa kwa uchangamfu ambapo watoto wameonyesha utayari wa kuanza darasa la kwanza huku akisisitiza wazazi kuandikisha watoto wenye utayari kuanza darasa la kwanza na awali Kwa ambao hawajapata utayari huku akitoa pongezi kwa Walimu Jamii (MJM) wa shule shikizi Pombwe Kuu, King’ongo na Uchembe kwa kazi nzuri inayoonekana kwani watoto wameonesha wapo tayari kuanza shule.
Kwa nyakati tofauti waheshimiwa madiwani, wenyeviti wa Vijijina Vitongoji wameshukuru program ya Shule Bora na Taasisi ya Elimu Tanzania Kwa kuanzisha mradi na kufuatilia kwa umakini, kwani uanzishwaji wa Madarasa ya utayari yamesaidia wazazi kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji Mali Kwa uhuru uwepo wa kituo cha utayari karibu unawapunguzia safari za kupeleka watoto shule na kuwafuata wakati wa kurudi majumbani.pia wameahidi kushirikiana na serikali pamoja na wananchi kuhakikisha vyumba vya Madarasa vinapatikana Katika maeneo ya karibu.
Kwa upande wake mwakilishi wa wananchi wa Pombwe Kuu ameomba Jengo la shule shikizi lifanyiwe maboresho huku akisema suala la eneo la Ujenzi wa shule wawaachie litapatikana.wakati huo huo wananchi wa kitongoji Cha King’ongo na kata ya Mjawa waneomba ngazi ya Taifa kuendelea kuwasemea ili kuisaidia upatikanaji wa maendeleo ya Elimu nchini hususani maeneo ya vijijini.
Zoezi la ufuatiliaji limeongozwa na Viongozi wa TET nchini, Wilaya ya Kibiti limefanyika katika kata ya Mjawa kituo cha utayari Uchembe na Kata ya Kiongoroni katika Kijiji cha Pombwe kuu na kitongoji cha King’ongo .
Shule bora ni mradi wa Serikali unaofadhiliwa na serikali ya Uingereza kupitia mfuko wake wa misaada UKAaid unaolenga kuinua kiwango cha elimu katika ngazi ya Elimu ya awali na msingi nchini ambapo jumla ya Mikoa tisa nchini ukiwemo Mkoa wa Pwani, kigoma,Dodoma, Tanga, Mara, singida,Rukwa, simiyu na katavi zitanufaika na mradi huo.
Katika ziara hiyo ya siku mbili Mratibu wa Programu ya Shule Bora Kutoka TET, iliambatana na Afisa Elimu Maalum wa Wilaya wa wanafunzi wenye uhitaji Maalum Shabani Makuka,yeye ametoa wito kwa jamii kuwafichua na kutowaficha watoto wenye ulemavu kwani Serikali inawatambua na kuwathamini kwa kuhakikisha wanapata Elimu kama wengine.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.