Shirika la Umeme TANESCO Wilaya ya Kibiti linaloongozwa na Meneja Safari Kubondoja limehitimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kuwatembelea na kuwashika mkono kina mama waliojifungua katika Hospitali ya Wilaya hiyo Upazi.
Vifaa walivyokabidhi ni sabuni ya unga katoni 2, sabuni ya kipande katoni 1, taulo za kike (pads) boksi 1kwa kinamama waliojifungua pamoja pambazi za watoto waliozaliwa katoni 1.
Kubondoja amesema katika kusheherekea siku hiyo ya huduma kwa wateja, wameona ni vema kushiriki pamoja na kinamama waliojifungua Hospitalini hapo kwani kwa kutoa kidogo walichojaliwa.
" Kwa umuhimu wa umeme, Watoto hawa waliozaliwa Hospitalini hapa ni wateja wetu wa baadaye" Alisema
Akijibu changamoto ya kukatikatika kwa umeme Wilayani humo Meneja huyo amesema wanaendelea kufanya maboresho kwa juhudi kubwa kwa kushirikiana na Wilaya zingine kuhakikisha wanatatua changamoto hiyo.
" Timu za Wilaya jirani zimekwisha wasili Kibiti na Sasa tunaweka nguzo za zege ambazo ni imara zenye uwezo wa kudumu mpaka miaka 50 bila kuharibika" Alisema Meneja.
Aidha amewashauri wananchi kuepuka tabia ya kuchoma moto kiholela kwani wengi wao husabanisha kuunguza nguzo zinazopelekea kutokea kwa hitilafu ya umeme, huku akishauri kuwa ni vema kutoa taarifa endapo kuna umuhimu wa kufanya hivyo ili waweze kuzuia changamoto zinazowezakutokea, ikiwa ni pamoja na kuingia kwa nguzo.
Katika zoezi hilo Meneja Kubondoja aliambatana na watumishi wa shirika Hilo, kutoka Idara ya uhasibu, mawasiliano na huduma kwa wateja pamoja na mafundi wa mitambo wa umeme
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.