Mratibu wa TASAF Mkoa wa Pwani Bi. Rose Kimaro amewasilisha taarifa juu ya utekelezaji wa shughuli za mpango wa kuzinusuru kaya masikini Mkoa wa Pwani katika kipindi cha Julai 2021- Juni 2023.
Bi Rose amewasilisha kwamba, utekelezaji umehusisha Halmashauri 9 za Mkoa wa Pwani zenye jumla ya vijiji 417 hadi kufikia Juni 2023 mwaka huu, tayari kaya 35,427 zimenufaika na mpango huo.
Vilevile Bi Kimaro amebainisha kuwa kwa kipindi cha Julai 2021 hadi Juni 2023, jumla ya sh. 2,027,497,054 zimetokewa ambapo sh.1,448,882,500 zimetolewa kwa ajili ya malipo na ununuzi wa vifaa na kiasi cha sh. 568,614, 500 zimetolewa kwa lengo la kutekeleza miradi 296 iliyoibuliwa katika Vijiji 224 na kutekelezwa na walengwa 10,907.
" Tunashukuru Serikali kwa kuanzisha mfumo huu, tangu uanze hadi sasa kwa Mkoa wa Pwani mafanikio ni makubwa katika nyanja mbalimbali na kaya nyingi zimepunguza umasikini kiuchumi na kijamii. ( Kuweka akiba, kupata ujira, kuboresha makazi ,kusomesha watoto, uhakika wa chakula n.k.).
Mbali na mpango kuwa na mafanikio makubwa, mratibu Rose amesema bado kuna changamoto mbalimbali zinawakabili kama vile kutokupokea ruzuku kwa kipindi kinachotakiwa, kucheleweshewa malipo ya walengwa, huku changamoto ikiwa ni kubaini sifa za wananchi kuingia kwenye mpango na kusababisha malalamiko kwa ambao hawajafanikiwa kuingia pamoja na kutokuwepo kwa uwazi na ukweli wa kaya zilizoimarika kuhitimu na kupisha walengwa wengine kuanza kunufaika.
Akijibu changamoto zilizobainishwa kwenye taarifa ya mkoa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Bi Grace Maghembe ameelekeza kusimamia na kuhakikisha malipo ya walengwa yanalipwa kwa wakati kuendana na kalenda ya malipo ili kuepuka malalamiko na kuboresha malengo kama yaliyokusudiwa.
" Jikiteni kwenye kuelimisha walengwa kutambua kuna kipindi malipo huchelewa kuepusha maswali mengi yenye sintofahamu fedha zikichekewa kuingia, hii itapunguza malalamiko" Alisema Dr.Maghembe.
Aidha Dr. Maghembe ameagiza kuimarishwa kwa mifumo ya kutunza taarifa ambazo zitasaidia kufuatilia na kutambua kaya zilizoimarika ili ziweze kuhitimu kwa wakati na kupisha kaya nyingine zinufaike.
"Mkiwa na utaratibu mzuri wa kufuatilia kimfumo utasaidia kuhakiki kaya zinazostaili kuhudumiwa na pamoja na kuwaingiza wananchi wenye sifa katika mpango huu" Alisema Maghembe.
" Pesa zitumike vizuri ili kila mwenye kaya duni anufaike, siyo mtu atake kunufaika milele, kuna watu wengi wanachangamoto, ningependa mkalisimamieni hilo."Alisema Maghembe.
Akijibu hoja ya kucheleweshwa kwa fedha za malipo Afisa wa Miradi TAMISEMI makao makuu Bw. Shambani Abdulmalik amesema amelichukua kikubwa ni kuimarisha mawasiliano ili kuweza kutatua tatizo kadri inavyowezekana.
Awali akikaribisha ugeni huo katika ukumbi wa Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Bw. Hemed Magaro, ameishukuru TASAF ujio wake na kazi nzuri za maendeleo wanazozifanya Wilaya ya Kibiti.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.