Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amefanya ziara ya kukagua shughuli za miradi ya Maendeleo Wilaya ya Kibiti ikiwa ni ziara ya siku 3 ndani ya Mkoa wa Pwani katika Halmashauri za Mkuranga, Kibiti na Kisarawe kuanzia Novemba 27-29 /2022.
Daraja hilo lenye urefu wa mita 61 mpaka linakamilika limetumia kiasi cha shilingi bil 7.2 fedha za Serikali Kuu ikiwa ni mkakati wa Serikali kuhakikisha kuwa wananchi wanahudumiwa mpaka vijijini.
Akiwa darajani hapo Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa amekagua na kuridhishwa na Mradi wa daraja la Mbuchi sambamba na kuipongeza TARURA kwa kazi nzuri ya kusimamia ujenzi wa daraja hilo.
Akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wananchi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge Kwa niaba wananchi wa mbuchi na Mbwera amemshukuru Rais kwa kukamilisha ujenzi wa daraja la mbuchi lilikuwa ni kilio cha muda mrefu Kwa wananchi wa eneo hilo .
Vilevile Mhe. Kunenge amesema eneo la Mbuchi ni la kimkakati kwa uchumi wa mkoa wa Pwani, kwani Kuna shughuli kubwa za kilimo na uvuvi zinazofanywa na wananchi Kwa ajili ya kujiongezea kipato na kuchagia Pato la serikali kwa ulipaji wa Kodi mbalimbali hivyo ukosefu wa daraja hilo kulizuia kufanyika kwa ufasaha shughuli hizo
Mhe.Waziri Mkuu amempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan Kwa kuunda taasisi ya wakala wa barabara TARURA Ili kuweza kukabili changamoto zote za barabara za mitaa na vijiji.
Waziri Mkuu amesema kukamilika Kwa daraja hilo ni neema Kwa wakazi wa Tarafa ya Mbwera kwani limekua kiunganishi na sasa panapitika Kwa msimu mzima na shughuli za uchumi zitaendelea na kuwataka wananchi kulinda miundombinu ya daraja hilo ili liweze kudumu.
Hata hivyo Waziri Mkuu amemwagiza Waziri wa Tamisemi kushughulikia barabara unganishi kutoka muhoro mpaka mbuchi.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewataka wafugaji kufuga kulingana na maeneo wanayoyamiliki, huku akiziagiza serikali za vijiji, wilaya na mkoa kutambua mifugo yote iliyopo na maeneo yao na kusimamia Kila mfugaji awe na eneo lake la kufungua. Pia amekemea mapigano ya wakulima na wafugaji na kutaka kuchukuliwe hatua kali za kisheria Kwa mfugaji ambaye hathamini maisha ya wengine.
Pia ameisisitiza utunzaji wa misitu ya mikoko na kuwataka wananchi wa mbuchi kutafuta njia nyingine za biashara na kujiinguzia kipato kwani ukataji wa mikoko utaathiri mazingira na vyanzo vya maji.
Nao wananchi wa Mbuchi na Mbwera Kwa nyakati tofauti wamemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa kutoa fedha za ujenzi wa daraja hilo kwani awali iliwalazimu kutumia mitumbwi ambayo ilikua tishio Kwa uhai hasa nyakati za Mvua pindi mto huo unapojaa maji.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.