Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Meja Edward Gowele, Mkurugenzi, Wakuu wa Idara mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti na Wananchi wa vijiji vya Nyambili na Nyambunda wameshiriki katika zoezi la kusomba mchanga wa ujenzi wa sekondari ya Nyambili Nyambuda katika kata ya Bungu.
Akiwa kwenye mkutano na wananchi waliofika katika eneo ambalo shule inajengwa ,Gowele amepongeza na kufurahishwa sana na kasi ya wananchi kwa namna wanavyojitoa kuhakikisha ujenzi wa shule hiyo unakamilika.
Vile vile Gowele akaagiza mipango kuanza kutafuta waalimu wa kufundisha shuleni hapo ianze mapema ,kwani shule hiyo inatakiwa kuanza kupokea wanafunzi ifikapo januari 2023, sambamba na zoezi la usajili wa shule ili iweze kutambulika.
Akijibu kero za wananchi kuhusu suala la mifugokuharibu Mazao yao, Mkuu wa Wilaya hiyo ameiagiza Idara ya Ardhi kupima na kutenga maeneo hayo kwa kuweka na kutambua mipaka ili kuepusha migogoro kati ya wakulima na wafugaji.
Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Ndg. Mohamed I. Mavura katika kuunga mkono juhudi za wakazi wa Nyambili Nyambunda kwa nguvu kazi waliyoionyesh, amesema Serikali itamalizia ujenzi wa madarasa matatu ambayo mpaka sasa yamefikia hatua ya boma kwa jitihada za wananchi.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya kibiti Ramadhan Mpendu [Diwani] na Katibu wa CCM Kata ya Bungu Hussein Tinge kwa nyakati tofauti wamempongeza Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa fedha za miradi mbalimbali anazoendelea kuzitoa kwa ajili ya miradi ya maendeleo Wilayani kibiti na Nchini kwa ujumla.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.