Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani Mohamed I. Mavura amefanya ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo katika Kata za Bungu na Mtawanya.
Akiwa katika Shule ya Msingi Kinyamale iliyopo katika kata ya Bungu, akajionea hali halisi ya ujenzi wa chumba cha darasa na ofisi ya walimu viko katika ngazi ya msingi huku katika kata ya Mtawanya, ujenzi wa darasa moja na ofisi unaendelea katika shule ya Msingi Roja ambapo darasa hilo liko katika hatua ya upauaji.
Mavura amesema "Ujenzi wa Madarasa uende sambamba na Ofisi za Walimu ili kupunguza changamoto za uhaba wa ofisi pamoja mrundikano wa walimu katika ofisi moja. Vilevile akawataka wasimamizi wa Miradi kuhakikisha kuwa wanatumia vizuri rasilimali zilizopo kama ilivyopangwa ili kuweza kufikia malengo na kukamilisha majengo kwa wakati uliopangwa.
Aidha,Mavura ameridhishwa na mradi wa Jengo la Wagonjwa wa dharula katika Hospitali ya Wilaya (EMD ) ambao upo katika hatua za mwisho na kumwagiza Muhandisi ahakikishe kasoro ndogo ndogo zilizopo zinatatuliwa haraka kabla Jengo halijaanza kutumia.
Miradi yote ya shule inaghalimu jumla ya milioni 40, ambapo Kila shule ni milioni 20 wakati Mradi wa Jengo la Wagonjwa wa Dharula ukigharimu takribani shilingi Milioni 300 za kitanzania.
Katika ziara hiyo ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo Mkurugenzi aliambatana na Kassim Mponda ambaye ni Mhandisi na Afisa Elimu Msingi wa Wilaya hiyo Mwalimu Zakayo Mlenduka.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.